• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa Kenya wakadiriwa kukua kwa asilimia 6.1 mwaka huu

    (GMT+08:00) 2020-01-23 10:57:23

    Wizara ya fedha ya Kenya inakadiria kuwa uchumi wa nchi hiyo utakua kwa zaidi ya asilimia 6.1 mwaka huu, kikiongezeka kutoka asilimia 5.6 za mwaka jana.

    Waziri wa fedha Bw. Ukur Yatani ameeleza kuwa ukuaji utaungwa mkono na sekta ya huduma yenye nguvu, mazingira ya kiuchumi yenye utulivu na uwekezaji unaoendelea chini ya mkakati wa "Ajenda Nne Kuu" za serikali.

    Bw. Yatani amesema, mwaka jana moja kati ya vyanzo vya kupungua kwa ukuaji wa uchumi ilikuwa ni kuchelewa kwa mvua kwenye nusu ya kwanza ya mwaka jana, kulikoathiri uzalishaji wa kilimo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako