Kocha wa Barcelona, Quique Setien amethibitisha timu hiyo kufanya usajili wa mshambuliaji mwingine mwezi huu baada ya mshambuliaji wake wa sasa Luis Suarez kupata maumivu yatakayomweka nje ya uwanja kwa muda mrefu. Barcelona inataka kumsajili mshambuliaji mpya huku ikimfuatilia nyota wa Arsenal, Pierre-Emerick Abumeyang ikiamini atafaa zaidi kuziba nafasi hiyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |