• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msimamo mkali wa kidini ni mzizi wa vitendo vya kigaidi mkoani Xinjiang

    (GMT+08:00) 2020-01-23 18:54:03

    Msemaji wa ofisi ya habari ya serikali ya mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uyghur wa China Yilijiang Anayiti amesema, msimamo mkali wa kidini ni mzizi wa vitendo vya kigaidi mkoani humo.

    Anayiti amesema, watu wenye msimamo mkali wa kidini wanachochea kupinga serikali kwa kisingizio cha kabila na dini, kuchukulia watu wasiokubali msimamo wao kama ni wapagani, na kuwafanya wafuasi wao wawe magaidi wanaodhibitiwa nao.

    Aidha, amekosoa kauli ya Gazeti la New York Daily la Marekani inayosema shule za bweni mkoani Xinjiang zimewaumiza wanafunzi kwa kuwatengenisha na wazazi wao. Amesema mkoa huo umeanzisha shule za bweni ili kupunguza mizigo ya familia ya wanafunzi, kwani mkoa huo una eneo kubwa, na vijiji vingi viko mbali na shule. Ameongeza kuwa nchi iliyoanzisha shule za bweni ni Uingereza, na hata Marekani pia ina shule nyingi za aina hiyo, inapaswa kujiuliza kama wanafunzi wao pia wameumia kutokana na shule hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako