• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kuendelea kuripoti maambukizi ya virusi vya nimonia kwa dunia

  (GMT+08:00) 2020-01-23 18:55:00

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China itaendelea kufuata msimamo wazi na wa kuwajibika kwa afya ya dunia, na kuendelea kuripoti juu ya maambukizi ya virusi vipya vya Korona vinavyosababisha ugonjwa wa nimonia kwa wakati.

  Bw. Geng ameyasema hayo alipoulizwa kuhusu mkutano wa kwanza wa kamati ya matukio ya dharura ya Shirika la Afya Duniani kuhusu maambukizi hayo. Amesema mtendaji mkuu wa WHO Tedros Ghebreyesus hajatangaza kama maambukizi ya virusi vipya vya Korona nchini China ni tukio la dharura la afya ya umma la kimataifa, na pande mbalimbali zitadumisha mawasiliano na ushirikiano wa karibu kuhusu hatua za kukabiliana na maambukizi hayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako