• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaripoti kesi 571 mpya zilizothibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Korona

    (GMT+08:00) 2020-01-23 19:16:53

    Kamati ya Taifa ya Afya nchini China imesema, hadi kufikia jumatano usiku, kesi 571 ya maambukizi ya virusi vya korona zimethibitishwa katika majiji na mikoa 25 nchini humo.

    Licha ya hayo, jumla ya kesi 393 zinashukiwa kuwa na maambukizi ya virusi hivyo vilivyosababisha vifo vya watu 17 katika mkoa wa Hubei ulioko katikati ya China.

    Mji wa Wuhan ambako virusi vya korona viligundulika kwanza, umetangaza hatua kadhaa ili kuzuia kuenea kwa virusi hivyo. Kuanzia leo saa nne asubuhi, safari za vivuko na mabasi ya safari ndefu zimesitishwa, na viwanja vya ndege na treni kwenda nje ya mji huo pia vimefungwa mpaka itakapoarifiwa. Wananchi hawaruhusiwi kutoka nje ya mji isipokuwa kwa sababu maalum, na wakazi wote wa mji huo wanatakiwa kuvaa barakoa wanapokuwa kwenye maeneo yenye watu wengi.

    Wakati huohuo, mamlaka nchini China zimetangaza hatua mfululizo za kuzuia na kudhibiti kuenea kwa virusi vipya vya korona.

    Wizara ya Fedha na Idara ya Taifa ya Kusimamia Usalama wa Afya nchini China zimetoa waraka unaoeleza kuwa ziko tayari kutoa msaada wa kifedha kwa kuwatibu wagonjwa waliopata maambukizi ya ugonjwa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako