• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mamlaka ya wanyamapori yakamata Simba 11 waliotoka kwenye hifadhi ya Serengeti

  (GMT+08:00) 2020-01-23 19:20:45

  Mamlaka ya wanyamapori nchini Tanzania imewakamata Simba 11 kati ya 16 waliotoka kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kusababisha vurugu kwa wakazi wa maeneo ya karibu na hifadhi hiyo.

  Ofisa wa ngazi ya juu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini Tanzania (TAWA) Bw. Edwin Njimbi amesema, Simba hao waliokamatwa wamewekwa kwenye visimba maalum. Amesema askari wa wanyamapori bado wanaendelea kuwatafuta na kuwakamata Simba wengine watano waliobakia.

  Amesema kazi ya kuwakamata Simba hao inafanywa na TAWA kwa kushirikiana na Hifadhi za Taifa za Tanzania na Kituo cha Utafiti wa Wanyamapori nchini Tanzania.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako