• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiongozi wa mkoa wa utawala maalum wa Hong Kong asisitiza umuhimu wa sera ya nchi moja na mifumo miwili huko Davos

    (GMT+08:00) 2020-01-23 19:20:47

    Kiongozi wa mkoa wa utawala maalum wa Hong Kong Bi. Carrie Lam jana alisisitiza umuhimu wa kuelewa kwa usahihi na kutekeleza kwa pande zote sera ya 'nchi moja na mifumo miwili', na kushikilia utawala wa kisheria kwa mustakabali wa mkoa huo.

    Bi Carrie alisema hayo wakati alipohudhuria mkutano wa baraza la uchumi la dunia huko Davos nchini Switzerland.

    Akiwa Davos, Kiongozi huyo alikutana na waziri mkuu wa Singapore Bw. Lee Hsien Loong na waziri mkuu wa Luxembourg Bw. Xavier Bettel, na kusema mkoa wa Hong Kong unakumbwa na changamoto kubwa ambayo haijawahi kutokea, na anaamini kuwa, mkoa huo una uwezo wa kushinda matatizo ya sasa kutokana na msingi wake imara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako