• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Mataifa waanzisha mpango wa "miaka 10 ya kivitendo" wa kutimiza lengo la maendeleo endelevu

  (GMT+08:00) 2020-01-23 19:21:10

  Umoja wa Mataifa jana ulianzisha rasmi mpango wa "miaka 10 ya kivitendo" wa kutimiza lengo la maendeleo endelevu, na kusisitiza kuharakisha kukabiliana na changamoto ngumu zaidi duniani ikiwemo umaskini na mabadiliko ya hali ya hewa, ili kuhakikisha kutimiza mswada wa maendeleo endelevu wa mwaka 2030 uliokuwa na malengo 17 ya maendeleo endelevu.

  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesisitiza kuhimiza mpango huo kwa pande tatu, ambazo ni kuanzisha hatua za kivitendo duniani, ili kuongeza nguvu ya uongozi, kuweka rasilimali nyingi zaidi na kuchukua utatuzi wenye busara zaidi, kuimarisha hatua za sehemu mbalimbali ili kufanya mageuzi ya sera, bajeti, muundo wa idara na usimamizi katika serikali, miji, na mitaa, kuanzisha harakati ya watu wote wakiwemo vijana, jamii ya umma, vyombo vya habari, sekta binafsi, vyama vya wafanyakazi, sekta ya wataalam na wadau wengine wanaohusika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako