• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkoa wa Xinjiang China waeneza elimu ya Kichina sanifu

  (GMT+08:00) 2020-01-23 19:42:40

  Mkurugenzi wa idara ya elimu ya eneo la Kashi mkoani Xinjiang, China Bw. Anwar Abulimit amesema, kwa kufuata kwa makini sheria ya elimu ya China, mkoa huo umeanzisha elimu ya Kichina sanifu, huku ukizingatia masomo ya lugha za makabila madogo.

  Bw. Abulimit amesema, kufundisha Kichina sanifu kutasaidia wanafunzi kuzoea zaidi katika jamii ya kisasa, kujifunza, kupata ajira na kufanya mawasiliano. Pia amesema, hivi sasa, wanafunzi wengi wameongeza uwezo wa kuongea Kichina sanifu na kuweza kusaidia wazazi wao kutafsiri na kuwasiliana na jamii za nje.

  Naye Meya wa mji wa Hetian, mkoani Xinjiang Bw. Rexiati Mushajiang amesema, habari zilizotolewa na vyombo vya habari vya nchi za magharibi zilizopaka matope elimu ya uzalendo mkoani humo ni sawa na kutumia vigezo viwili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako