• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi asisitiza kukimbizana na wakati ili kutimiza Ndoto ya China

  (GMT+08:00) 2020-01-23 19:44:46

  Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kukimbizana na wakati na kuambatana na historia ili kutimiza Ndoto ya China ya Ustawishaji wa Taifa.

  Rais Xi ametoa kauli hiyo alipohutubia sherehe ya kukaribisha Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina leo hapa Beijing.

  Rais Xi pia amesema wakati na historia havisubiri mtu lakini vinamilikiwa na watu wenye bidii. Ameongeza kuwa chini ya uongozi imara wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC, wanachama wote wa CPC, wanajeshi wote na watu wa makabila mbalimbali, wanatakiwa kutoogopa upepo au mawimbi, bali kushindana moja kwa moja na changamoto na kusonga mbele kuelekea lengo zuri la ustawishaji wa kitaifa na mustakbali mzuri wa kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako