• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Tanzania amfuta kazi waziri wa mambo ya ndani kwa wizara hiyo kuongoza kwa miradi ya udanganyifu

  (GMT+08:00) 2020-01-23 20:25:29

  Rais wa Tanzania John Magufuli amemfuta kazi Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo Kangi Lugola, akisema wizara hiyo inaongoza katika kuchukua miradi ya ovyo.

  Rais Magufuli pia amemfuta kazi Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini humo, Thobias Andengenye kwa kusimamia mradi usieleweke wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 452.

  Rais Magufuli alitangaza kuwafuta kazi viongozi hao wawili muda mfupi baada ya kuzindua mradi wa nyumba za maofisa magereza katika mji wa kibiashara wa Dar es Salaam.

  Amesema naibu waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni na katibu mkuu wa wizara hiyo Jacob Kingu wamemwandikia barua ya kujiuzulu nyadhifa zao na amezipokea.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako