• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu 830 wathibitishwa kuambukizwa virusi vipya vya nimonia aina ya 2019-nCoV

  (GMT+08:00) 2020-01-24 10:00:52

  Habari kutoka kamati ya usafi na afya ya China zinasema, hadi saa 6 usiku wa tarehe 24, watu 830 walithibitishwa kuambukizwa virusi vipya vya nimonia aina ya 2019-nCoV kote nchini China ambao 177 kati yao wako katika hali mbaya, 25 wamefariki dunia. Wengine 34 waliothibitishwa kuambikizwa virusi hivyo wamepona.

  Waliothibitishwa kuambukizwa virusi hivyo nje ya China bara ni pamoja na watu wawili wa Hongkong na Macao, mmoja Taiwan, watu watatu nchini Thailand ambao wawili wamepona, watu wawili Viet Nam, mtu mmoja Marekani, Korea Kusini na Singapore, mtu mmoja Japan ambaye amepona.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako