• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM yatoa dola milioni 10 kwa ajili ya dawa ya kupuliza kuuza nzige

    (GMT+08:00) 2020-01-24 17:00:05

    Naibu msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema umoja huo umetoa dola za kimarekani milioni 10 kwa ajili ya kupuliza dawa ya kuua nzige, mlipuko ambao ni mkubwa kutokea katika Afrika Mashariki kwa miongo kadhaa.

    Akifafanua kuhusu mlipuko huo, Bw. Haq amesema wadudu hao wanaathiri pembe ya Afrika, Asia kusini mashariki na Bahari nyekundu, na kwamba kwa upande wa Ethiopia, Somalia na Kenya hali ni mbaya zaidi kushuhudiwa katika miaka 70 iliyopita. Amesema mazao yanateketea kwenye jamii ambazo tayari zinashuhudia upungufu wa chakula. Mlipuko huo umekuwa mbaya zaidi ikiwa ni matokeo ya mabadiliko ya tabianchi tayari yanaonekana katika kanda hii.

    Fedha hizo zitakwenda kwenye Shirika la Chakula na Kilimo FAO, ambalo litazitoa kwa ajili ya operesheni ya kupuliza dawa ya kuua nzige hao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako