• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Mataifa watafuta dola bilioni moja kusaidia Somalia katika mwaka 2020

  (GMT+08:00) 2020-01-24 17:01:00

  Umoja wa Mataifa unatafuta dola za kimarekani bilioni moja ili kusaidia operesheni za kibinadamu nchini Somalia katika mwaka 2020.

  Hayo yamesemwa na naibu msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq. Amefafanua kuwa umoja huo pamoja na serikali ya Somalia na washirika wake wa kibinadamu, wameanzisha mwitikio wa kibinadamu mwaka 2020 katika nchi hiyo ya pembe ya Afrika. Amesema pesa zitatumika kutoa msaada wa kuokoa maisha na msaada wa maisha kwa watu milioni 3, ambapo karibu nusu ni wakimbizi wa ndani.

  Hata hivyo, kulingana na Umoja wa Mataifa watu wapatao milioni 5.2 wa Somalia wanahitaji msaada wa kibinadamu, wakiwemo milioni 1.7 waliokimbia makazi yao kutokana na migogoro, hali ya kutokuwa usalama, waliohamishwa kwa nguvu, ukame, na mafuriko.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako