• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bw. Guterres asema ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu inapaswa kuwa mpango mkuu wa maendeleo ya kila nchi

  (GMT+08:00) 2020-01-24 17:01:27

  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres jana alisema kwamba ajenda ya mwaka 2030 ya Maendeleo Endelevu, ambayo imepitishwa mwaka 2015, inapaswa kuwa mpango mkuu wa maendeleo ya kila nchi, na vilevile iwe muhimu kwa biashara.

  Akiongea kwenye mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Kiuchumi la Dunia WEF, Bw. Guterres amesema inatia moyo kuona WEF ipo mstari wa mbele kwenye juhudi hizi kuweka asasi za kijamii, serikali na wafanyabiasha kushirikiana pamoja, ili kuhakikisha kwamba wanatumia faida zote duniani, na kufanya kwa njia ambayo kila mmoja ananufaika.

  Amesisitiza kuwa kuna mengi yanayohitaji kufanywa ili kuhamasisha jamii ya kimataifa kufanya Malengo ya Maendeleo Endelevu kuwa halisi, na kutoa wito wa kuongezwa juhudi, na kujitolea kwa moyo kuhamasisha rasilimali, hasa fedha kwa ajili ya mabadiliko ya tabianchi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako