• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CMG yaonesha tamasha la sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina

    (GMT+08:00) 2020-01-24 20:23:30

    Leo tarehe 24 ni mkesha wa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina. Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG linaonesha tamasha kubwa lililotumia teknolojia mpya za mtandao wa 5G na drone, ili kufurahisha watu wa dunia nzima.

    Tamasha hilo lenye dakika 260 limejumuisha maonesho mbalimbali yakiwemo ngonjera, nyimbo, ngoma, opera, viinimacho, na sarakasi. Maandalizi ya tamasha hilo yametumia sayansi ya kisasa zikiwemo roboti na drone, na kwa mara ya kwanza limetangazwa kwa teknolojia ya VR.

    Pamoja na Beijing, tamasha hilo pia litakuwa na majukwaa mkoani Henan na katika sehemu ya ghuba kubwa ya Guangdong, Hong Kong na Macao, ili kuonesha utamaduni wa sehemu mbalimbali.

    Licha ya tamasha hilo kupitia televisheni, CMG pia limetengeneza filamu ya "Tamasha la mwaka 2020 la sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina", na kuieneza katika zaidi ya vyombo vya habari 500 vya zaidi ya nchi na sehemu 170, zikiwemo Marekani, Uingereza, Japan, Russia, Brazil, Singapore, Falme za Kiarabu, Malaysia, Thailand na Laos.

    Tamasha la sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina lilianzishwa mwaka 1983 na Shirika la Kitaifa la Televisheni la China ambalo sasa liko chini ya Shirika Kuu la Utangazaji la China. Katika zaidi ya miaka 30 iliyopita, kila mwaka Wachina wanasherehekea mkesha wa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi kwa kutazama tamasha hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako