• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaunga mkono pendekezo la Russia la kuitisha mkutano wa kilele wa nchi wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama

  (GMT+08:00) 2020-01-24 17:50:49

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema China inaunga mkono pendekezo lililotolewa na rais wa Russia la kuitisha mkutano wa kilele wa nchi wanachama watano wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

  Rais Vladmir Putin wa Russia alitoa pendekezo hilo tarehe 23 kwenye kongamano la tano la kimataifa la mauaji makubwa lililofanyika huko Jerusalem.

  Bibi Hua amesema huu ni mwaka wa 75 tangu ushindi wa vita dhidi ya Ufashisti na kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, na kwamba nchi wanachama wa kudumu kufanya mawasiliano ya kina na kuongeza uratibu na ushirikiano kuhusu hali ya kimataifa na masuala muhimu ya kimataifa, kuna maana kubwa katika kulinda utaratibu wa pande nyingi na utaratibu wa kimataifa baada ya vita vikuu vya pili vya dunia, na pia ni muhimu katika kulinda mamlaka ya Umoja wa Mataifa, amani na utulivu wa kimataifa na kikanda.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako