• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: TRA yaboresha mifumo ya kupokea taarifa

  (GMT+08:00) 2020-01-24 19:26:21
  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema imeboresha mifumo ya kupokea taarifa na uchakataji kwa lengo la kuondoa malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara wakati wa ukadiriaji wa kulipa kodi.

  Imesema imekuwa ikitoa mafunzo ya ukadiriaji kodi kwa wafanyakazi wake ili kumwezesha mfanyabiashara alipe kodi ya biashara yake kwa uhalali.

  Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Msafiri Mbibo, aliyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati mkutano kati ya wafanyabiashara wakubwa na TRA uliolenga kuboresha uhusiano kati yao.

  Alisema TRA pia imeweza kuboresha uhusiano na wafanyabiashara wakubwa kwa kuwa nao karibu wakati wote.

  Aidha, alisema vigezo vinavyotumika kuwatenganisha wafanyabiashara wadogo, wakati na wakubwa ni mapato ghafi yanayozalishwa na mfanyabiashara, viwango vya ajira vinavyotolewa na mfanyabiashara.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako