• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda: Uganda kuuza samaki China

  (GMT+08:00) 2020-01-24 19:26:41
  Waziri Uvuvi wa Uganda Bi Hellen Adoa, amesema nchi hiyo iko tayari kuanza kuuza wa samaki wa moja kwa moja kwenda China.

  Alisema wanatarajia kuanza kuuza samaki kwenye soko hilo mwezi Februari mwaka huu baada ya nchi hizo mbili kutia saini mkataba wa maelewano (MoU).

  Alisema waziri huyo kuwa wanakadiria mauzo ya kila mwaka yatakuwa tani 520.

  Waziri huyo alionya kuwa wale wanaoshindwa kukidhi mahitaji ya chini ya usindikaji wa samaki, watapokonywa leseni na maduka yao kufungwa.

  Uganda inazalisha hadi tani 447,020 za samaki kila mwaka kutoka vyanzo vya maziwa mito na ufugaji.

  Samaki aina Nile Perch huchangia karibu tani 86,463 ya uzalishaji wa jumla, nayo tilapia tani 49,768.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako