• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Tanzania yauza asilimia 80 ya pamba yake nje ya nchi

  (GMT+08:00) 2020-01-24 19:32:18

  Tanzania imeuza nje asilimia 80 ya pamba katika msimu uliopita.

  Naibu waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, ameagiza kampuni 23 ambazo zilinunua pamba kwa wakulima kuwasilisha taarifa za mauzo kabla ya Januari 31, mwaka huu.

  Bashe alitoa kauli hiyo katika mkutano baina ya wanunuzi wa pamba, wauzaji pembejeo na taasisi za kifedha uliofanyika jijini hapa.

  Alieleza kuwa kampuni hizo zilinunua pamba tani 350,000 msimu huo chini ya usimamizi wa serikali.

  Aidha, Naibu Waziri huyo alisema kuwa msimu ujao wa mavuno ya pamba malipo yote yatafanyika kupitia benki na si kulipana mkononi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako