• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Klopp ana imani kwamba majeruhi aliyopata Sadio Mane sio makubwa atarejea Uwanjani hivi karibuni

  (GMT+08:00) 2020-01-24 19:33:44

  Kocha Mkuu wa Liverpool Jurgen Klopp ana matumaini kwamba majeruhi aliyopata mshambuliaji wake Sadio Mane sio makubwa sana na atarejea Uwanjani hivi karibuni. Mane aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Wolves, Jana, Januari 23, kipindi cha kwanza baada ya kucheza dakika 30 na nafasi yake ilichukuliwa na Takumi Minamino, mshambuliaji mpya wa Liverpool aliyekuwa benchi. Mchezo dhidi ya Wolves unakuwa ni wa kwanza kwa Mjapani Minamino kucheza ndani ya Ligi Kuu England baada ya kuingia mkataba ndani ya timu hiyo akitokea Red Bull Salzburg. Liverpool ilishinda kwa jumla ya mabao 2-1 kwenye mchezo huo ambapo mabao ya Liverpool yalifungwa na Jordan Henderson kwa kichwa dakika ya nane na lilisawazishwa dakika ya 51 na Wolves kupitia kwa Raul Jimenez dakika ya 51 na lile la ushindi likipachikwa na Roberto Firmino kwa Liverpool dakika ya 84.

  Ushindi huo unaifanya Liverpool kufikisha jumla ya pointi 67 ikiwa kileleni, ikiwaaacha kwa tofauti ya pointi 16 mabingwa watetezi Manchester City wenye pointi 51 huku Wolves ikiwa nafasi ya 7 na pointi zake 34.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako