• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Daniel James awaomba radhi mashabiki wa Manchester United baada ya kupokea kipigo dhidi ya timu ya Burnley

  (GMT+08:00) 2020-01-24 19:34:38

  Daniel James amewaomba radhi mashabiki wa Manchester United baada ya kupokea kipigo dhidi ya timu ya Burnley hapo juzi siku ya Jumatano. Winga huyo wa United, amesema kuwa pafomansi ya timu yao haikuwa nzuri na kuahidi kufanya vizuri katika michezo ijayo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amesema kama timu, wanahitaji kuwa katika nafasi nzuri, walilenga langoni mashuti mengi, pengine walipaswa kufunga bao kutokana na nafasi walizotengeneza. United ilipoteza mchezo huo wakiwa nyumbani katika uwanja wa Old Trafford kwa jumla ya mabao 2 – 0 dhidi ya Burnley, magoli yakifungwa dakika ya 39 na 56 kupitia Chris Wood na Jay Rodriguez.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako