• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Tepsi Evance awasili nchini Ufaransa ili kujiunga na timu ya Nantes

  (GMT+08:00) 2020-01-24 19:37:28

  Nyota wa timu ya vijana ya Azam FC 'Azam U-20' na timu ya Taifa ya Vijana 'Ngorongoro Heroes', Tepsi Evance, amewasili nchini Ufaransa kwa ajili ya kujiunga na timu ya Nantes. Tepsi aliondoka juzi pamoja na wakala anayetambulika na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Kambi Seif kwenda Nantes kwa ajili ya mafunzo hadi atakapotimiza umri wa miaka 18 baadae mwaka huu asaini mkataba. Evance atakapofikisha umri huo, atajiunga moja kwa moja na timu ya wakubwa ya Nantes inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo (Ligue 1). Tepsi ni mmoja kati ya vijana wanne waliopatikana kwenye usaili uliofanywa na Cambiasso Sports na Rainbow Sports Novemba mwaka jana, kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Mchezaji mwingine wa Azam U-20, aliyefuzu kwenye usaili huo ni nahodha, Samuel Onditi, ambaye anasubiria taratibu za Viza zikamilike sambamba na wachezaji wengine wawili.

  Wakati huohuo Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amempongeza Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta kwa kufanikiwa kujiunga na Timu ya Aston Villa

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako