• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tamasha la Spring Festival laonesha moyo wa kujitahidi walio nao wachina katika zama mpya

    (GMT+08:00) 2020-01-25 18:41:48

    Jana saa 2 jioni kwa saa za Beijing, tamasha la kusherehekea mwaka mpya wa jadi wa kichina yaani Spring Festival limeonyeshwa nchini China.

    Tamasha hilo lililoandaliwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG likwa na kauli mbiu ya "kutimiza ndoto ya kujenga jamii yenye maisha bora na kusherehekea mwaka mpya wa jadi kwa furaha" linajumuisha maonesho mbalimbali yakiwemo ngonjera, nyimbo, ngoma, opera, viinimacho, na sarakasi. Wakati huohuo, tamasha la jana pia liliwafuatilia wauguzi na wananchi wanaokabiliwa moja kwa moja na maambukizi ya virusi vya korona vya aina mpya vinavyosababisha homa ya mapafu, na kuwapa imani na njia imara katika juhudi zao za kuyashinda.

    Kiwango cha watazamaji wa tamasha la Spring Festival la mwaka huu kimeongezeka sana kuliko miaka iliyopita. Kwa mujibu wa takwimu zisizokamilika, hadi kufikia saa sita usiku wa tarehe 24, watu waliotazama tamasha hilo moja kwa moja kwenye mtandao wa internet walifikia bilioni 1.1, na waliolitazama kwenye televisheni walifikia milioni 589. Aidha, vyombo vya habari vya nje zaidi ya 560 vimetangaza au kuripoti tamasha hilo, ambapo tamasha hilo liliwafikia watu zaidi ya milioni 24.62 kwenye mitandao ya Youtube na Facebook.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako