• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Naibu waziri mkuu wa China ataka kuwepo uwazi katika vita dhidi ya virusi vya korona

  (GMT+08:00) 2020-01-25 18:42:20

  Naibu waziri mkuu wa China Sun Chunlai ametoa wito wa kuwepo uwazi na hisia ya dharura katika vita vigumu dhidi ya mlipuko wa virusi vya korona vya aina mpya mjini Wuhan, mkoani Hubei, katikati ya China.

  Bibi Sun ametoa kauli hizo alipohudhuria mikutano ya baraza la serikali la kuzuia na kudhibiti mlipuko huo, iliyofanyika Jumatatu, Alhamisi na Ijumaa. Akizungumzia kuenea kwa virusi hivyo, Sun amezitaka serikali za mitaa na idara husika kuwajibika zaidi na kuchukua hatua kali na lengwa ili kuzuia virusi hivyo.

  Habari nyingine zinasema China imetuma madaktari wanajeshi 450 wakiwemo wale bingwa wenye uzoefu katika kupambana na maambukizi ya virusi vya SARS na Ebola kwenda mjini Wuhan. Wanajeshi hao wakiwa katika timu tatu ambazo ni madaktari wa magonjwa ya kupumua, magonjwa ya kuambukiza na kitengo cha wagonjwa mahututi watapelekwa hospitali za Wuhan zenye wagonjwa wengi wa nimonia zinazosababishwa na virusi vya korona vya aina mpya.

  Mamlaka za afya za China zimetangaza kuwa hadi sasa watu zaidi ya 1,300 wamethibitishwa kuambukizwa virusi hivyo.

  Wakati huohuo daktari wa magonjwa ya kupumua Zhong Nanshan anayeongoza jopo la madaktari wa Idara ya Afya ya Taifa ya China, amesema dawa kadhaa zitatumika kwenye majaribio ya kimatibabu ya ugonjwa huo, na kusisitiza kuwa usalama wa dawa umehakikishwa, lakini ufanisi wake bado unahitaji kuthibitishwa zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako