• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi aendesha mkutano wa kujadili kazi za kukinga na kudhibiti nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona

  (GMT+08:00) 2020-01-25 21:20:52

  Rais Xi Jinping wa China ameendesha mkutano wa kusikiliza kazi za kukinga na kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa nimonia unaosababishwa na virusi vipya vya korona leo hapa Beijing, ambao umefanya utafiti tena, kupanga upya na kuhamasisha zaidi kazi hizo haswa jinsi ya kuwatibu wagonjwa.

  Mkutano huo ulioitishwa na Idara ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China umeamua kuwa Kamati kuu hiyo itaunda timu ya uongozi ya kazi za kukabiliana na maambukizi hayo, na kutuma vikundi vya uongozi kwenye sehemu zenye maambukizi mabaya mkoani Hubei ili kuimarisha kazi za kukinga na kudhibiti katika mstari wa mbele.

  Kwenye mkutano huo, rais Xi amezitaka kamati za chama na serikali za ngazi mbalimbali ziweke kipaumbele maisha na afya ya wananchi na kuzifanya kazi za kukinga na kudhibiti maambukizi hayo kuwa kazi za msingi kwa hivi sasa. Pia amezitaka zitambue umuhimu na udharura wa kazi za kukinga na kudhibiti maambukizi hayo, kuhakikisha dawa na rasilimali za kutosha na kuimarisha ulinzi wa usalama wa wauguzi.

  Aidha, mkutano huo umesisitiza kuwatibu wagonjwa kwa nguvu zote, kufanya kazi za kukinga na kudhibiti maambukizi kwa njia ya kisanyansi na taratibu. Vilevile, mkutano huo umetaka kutoa ripoti za maambukizi hayo kwa usahihi na uwazi ili kujibu ufuatiliaji wa ndani na nje ya China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako