• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu bilioni 1.232 watazama tamasha la mwaka mpya wa jadi wa kichina la CMG

    (GMT+08:00) 2020-01-26 19:28:21

    Tamasha la mwaka mpya wa jadi wa kichina lililoandaliwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG lilitangazwa kwa mafanikio tarehe 24 ikiwa mkesha wa mwaka mpya, na kuvunja rekodi ya utangazaji kati ya vyombo tofauti vya habari.

    "Mara ya kwanza" nyingi zilizoonekana katika tamasha hilo la mwaka huu zimeonyesha wajibu na majukumu ya vyombo vya habari vya serikali ya China, pamoja na mvuto, uchangamfu na ubunifu wake katika zama mpya.

    Takwimu zimeonesha kuwa katika mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa kichina, channel 225 za televisheni zimetangaza tamasha hilo moja kwa moja nchini China, na katika nchi za nje vyombo vya habari karibu 600 kutoka nchi na sehemu 170 duniani vimeripoti tamasha hilo. Idadi ya watazamaji waliolitazama tamasha hilo moja kwa moja kwenye televisheni, internet na mitandao ya kijamii imefikia bilioni 1.232, na asilimia 98.65 ya watamazaji wameeleza kuridhika na tamasha hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako