• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kobe Bryant afariki kwenye ajali ya helikopta

  (GMT+08:00) 2020-01-27 16:37:29

  Dunia imekumbwa na mshtuko baada ya kupokea habari za nyota wa kikapu Black Mamba Kobe Bryant na binti yake Gianna "GiGi" Maria-Onore wamefariki dunia kwenye ajali ya helikopta binafsi iliyotokea jana Januari 26 Calabasas, California. Kwenye helikopta hiyo iliyokuwa na watu tisa, walikuwemo Kobe, binti wa Kobe, Gianna "GiGi" mwenye miaka 13, rafiki yake GIGI, mzazi wa rafiki yake GIGI, na abiria wengine wanne pamoja na rubani. Kobe Bryant aliyezaliwa Agosti 23 mwaka 1978 amefariki akiwa na umri wa miaka 41, na ameichezea timu ya mpira wa kikapu ya Los Angeles Lakers nchini Marekani kwa takribani miaka 20, hadi alipostaafu mwezi Aprili mwaka 2016.

   

  Kobe alikuwa mchezaji katika timu ya magwiji wa NBA Lakers mara 18, na mara 12 katika timu ya All-Defensive na pia Mchezaji Bora MVP mwaka 2008. Akiaminika kuwa mmoja wa wacheza basketball bora wa muda wote, aliongoza kwa kuwa mfungaji bora kwa misimu miwili, na alikuwa mfungaji bora wa nne katika ligi zote na mchezaji pekee katika nafasi ya Guard aliyecheza misimu 20 mfululizo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako