• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM wataka kuchukuliwa hatua za haraka kudhibiti uvamizi wa nzige nchini Ethiopia, Kenya na Somalia

    (GMT+08:00) 2020-01-27 19:27:39

    Ofisi ya Kuratibu Mambo ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa UNOCHA, imetaka kuchukuliwa kwa hatua za haraka za kudhibiti wakati ambapo Ethiopia, Kenya na Somalia zikiwa zimevamiwa na wimbi la nzige wa jangwani ambalo ni janga kubwa kushuhudiwa na nchi hizo tatu katika historia.

    Kwenye taarifa yake UNOCHA imesema nzige hao wameteketeza mamia ya kilomita za mashamba ya mboga nchini Ethiopia na makumi ya maelfu ya ekari za ardhi ya Somalia. Taarifa hiyo imesema nchini Kenya nzige kadhaa wamefika maeneo ya Rift Valley, na kubainisha kuwa bila ya kuchukuliwa hatua za haraka za kuzuia, kuna hatari kubwa ya nzige hao kufika kaskazini mashariki mwa Uganda, kusini mashariki mwa Sudan Kusini na kusini magharibi mwa Ethiopia.

    Wiki iliyopita Mfuko wa Mwitikio wa Dharura wa Umoja wa Mataifa ulitoa dola za Kimarekani milioni 10 kusaidia juhudi za kudhibiti nzige hao Afrika Mashariki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako