• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Sudan yasaini makubaliano ya Amani na makundi ya upinzani

  (GMT+08:00) 2020-01-27 19:28:00

  Serikali ya Sudan imesaini makubaliano ya Amani na makundi mawili ya upinzani kutoka Kaskazini mwa Sudan huko mjini Juba.

  Kwenye taarifa iliyotolewa jana na Baraza la Utawala la Sudan, makundi hayo ya Kush Movement na Northern Entity ni sehemu ya kundi la Revolutionary Front Alliance. Makubaliano hayo yanashughulikia masuala kadhaa yakiwemo ardhi na maendeleo pamoja na matatizo yanayowakabili watu walioathirika na ujenzi wa mabwawa.

  Akinukuliwa kwenye taarifa hiyo, mjumbe wa baraza la utawala la Sudan na msemaji wa serikali wa ujumbe wa mzungumzo, amesema kusainiwa kwa makubaliano hayo ya mwisho kunaonesha hatua kubwa zaidi kuelekea makubaliano ya kina ya amani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako