• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa WHO: hakuna haja kwa nchi za nje kuwaondoa watu China ili kuepuka maambukizi ya virusi vya korona

    (GMT+08:00) 2020-01-28 16:12:47

    Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema WHO haiungi mkono baadhi ya nchi kuwaondoa wananchi wao nchini China ili kuepuka maambukizi ya virusi vipya vya korona mjini Wuhan, China na kwamba WHO ina imani na uwezo wa China katika kuzuia na kudhibiti maambukizi hayo.

    Bw.Tedros amesema hayo alipokutana na waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi leo hapa Beijing. Amesema baada ya kutokea kwa maambukizi ya nimonia yaliyosababishwa na virusi vya korona, China ilitambua virusi ndani ya muda mfupi na kuifahamisha WHO na nchi nyingine kuhusu utaratibu wa jeni za virusi, na tena rais Xi Jinping wa China na serikali yake wanatilia maanani sana kukinga na kudhibiti maambukizi hayo, WHO na jumuiya ya kimataifa inashukuru juhudi kubwa hizo zinazofanywa na China katika kuzuia kuenea kwa virusi hivyo.

    Ameongeza kuwa WHO inapenda kutoa ushirikiano na msaada wote wa lazima unaohitajika kwa China.

    Bw. Wang Yi amesema China inapongeza WHO kwa kutambua juhudi mbalimbali za China katika kupambana na virusi vya korona kwa msimamo wa haki na usio na upendeleo. Amesema ziara hii ya Bw. Tedros sio tu imeonesha uungaji mkono wa WHO kwa China, bali pia itatoa nguvu kwa China na WHO kuongeza ushirikiano. Ameeleza matumaini yake kuwa ataweza kujionea nia thabiti ya serikali ya China na wananchi wake katika kupambana na virusi hivyo.

    Bw. Wang amesisitiza kuwa kutokana na uongozi imara wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China kiini chake akiwa rais Xi Jinping, manufaa ya mfumo wa ujamaa na uzoefu mzuri wa kupambana na virusi vya SARS uliopatikana miaka 17 iliyopita, China ina uwezo, imani na rasilimali za kutosha za kushinda maambukizi hayo.

    Bw. Wang ameongeza kuwa China itaendelea kushirikiana na jumuiya ya kimataifa haswa WHO kwa msimamo wa uwazi na kuchangia maendeleo ya shughuli za afya ya umma duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako