• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sofia Kenin na Ashleigh Barty kukutana kwenye nusu fainali ya michuano ya wazi ya Australia

  (GMT+08:00) 2020-01-28 18:15:05

  Mmarekani Sofia Kenin amefikia hatua ya nusu fainali ya Grand Slam kwa upande wa wanawake kwa kumshinda Mtunisia Ons Jabeur kwenye michuano ya wazi ya Australia. Kenin alimtoa Mmarekani Coco Gauff kwenye raundi iliyopita, na kushinda 6-4 6-4. Mchezaji namba 78 duniani Jabeur, ambaye ni mwanamke wa kwanza mwarabu kufikia robo fainali ya Grand Slam, ameonesha moyo mkubwa wa kupambana na kuokoa pointi tano kwenye seti ya kwanza kabla ya kumpa kibano cha nguvu kwenye seti ya pili, lakini mwishowe aliambulia kichapo na kutolewa na Kenin. Naye Ashleigh Barty amekuwa Muastralia wa kwanza mwanamke kufika nusu fainali ya Grand Slam inayofanyikia nyumbani kwa miaka 36 kwa kumshinda Petra Kvitova huko Melbourne kwa seti 7-6 (8-6) 6-2. Barty ambaye ni bingwa wa michuano ya wazi ya Ufaransa atavaana na Sofia Kenin ili kuwania nafasi ya kucheza fainali siku ya Jumamosi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako