• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kilimo cha pamba chazidi kusambaratika Lamu

    (GMT+08:00) 2020-01-28 19:01:46
    Zaidi ya wakulima 10,000 wa pamba, Kaunti ya Lamu wanahofia kusambaratika kwa kilimo hicho ambacho kimekuwa kikididimia kila kuchao katika siku za hivi karibuni.

    Tangu jadi, kilimo cha pamba kaunti ya Lamu kimekuwa kikiendelezwa kwa wingi kwenye maeneo ya Baharini, Tewe, Uziwa, Hongwe, Nairobi Area, Mpeketoni na kwenye maeneo ya Witu, Hindi na Faza.

    Katika mazungumzo na wanahabari wakati wa kongamano la kujadili muelekeo wa kilimo cha pamba Lamu, msemaji wa wakulima wa pamba eneo hilo, Joseph Migwi alisema kilimo cha pamba kwa sasa kimedidimia kwa hadi asilimia 30.

    Alisema kati ya wakulima zaidi ya 10,000 ambao wamekuwa wakiendeleza kilimo hicho Lamu, ni wakulima takriban 6000 pekee ambao bado wameshikilia kilimo cha pamba.

    Alisema wengi wao wamekuwa wakitekeleza kilimo cha kadri ambacho hakiwezi kukimu kiwango cha kibiashara.

    Alitaja wadudu ambao wamekuwa wakihangaisha wakulima kwa kuharibu mmea huo mashambani na ukosefu wa kiwanda cha pamba eneo la Lamu kuwa sababu kuu zinazochangia kufifia kwa kilimo hicho.

    Aliitaka serikali na wadau kujitokeza kusaidia kuboresha miundomsingi ya kilimo cha pamba ili sekta hiyo iweze kupanuliwa siku za usoni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako