• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya yaapa kuzidisha mapambano dhidi ya biashara ya magendo na haramu ili kupambana na ugaidi

  (GMT+08:00) 2020-01-28 19:31:20

  Serikali ya Kenya imeapa kuzidisha mapambano dhidi ya biashara ya magendo na haramu ikiwa sehemu ya mkakati wake wa kina wa kupambana na ufadhili wa ugaidi.

  Kemeo hilo lilitolewa jana na waziri wa mambo ya ndani wa Kenya Fred Matiang'i na kulaani vikali vitendo hivyo viovu ambavyo vinaumiza biashara nchini kwa kuwa wote wanaojihusisha na biashara hiyo wanawafadhili magaidi. Matiang'i amesema mashirika ya usalama yataanzisha haraka operesheni na kudumisha uchunguzi mipakani ili kusimamisha na kuzuia mtiririko wa bidhaa haramu, huduma na wahamiaji nchini.

  Mapema mwezi huu rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alivielekeza vyombo vya vya usalama nchini kuzuia njia zote ambazo al Shabaab wanatumia kupokea fedha kupitia Kenya, hasa kupitia magendo na biashara haramu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako