• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda kuandaa mkutano wa kilele wa kuzuia malaria na Magonjwa Yanayopuuzwa ya Tropikali

    (GMT+08:00) 2020-01-28 19:32:17

    Rwanda imechaguliwa kuandaa mkutano wa kilele wa kuzuia malaria na Magonjwa Yanayopuuzwa ya Tropikali utakaofanyika Juni 25 mwaka huu.

    Akiongea kwenye uzinduzi wa maandalizi ya mkutano huo mjini Kigali, waziri wa afya wa Rwanda Diane Gashumba amesema mkutano huo utatoa tahadhari kimataifa na kuchochea hatua za kumaliza magonjwa haya yanayozuilika lakini mara nyingi yanaua ambayo yamekuwa yakiwakumba binadamu kwa maelfu ya miaka.

    Kwa upande wake mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani WHO nchini Rwanda, Kasinde Mwinga, amesema kudhibiti na kutokomeza malaria na Magonjwa Yanayopuuzwa ya Tropikali ni msingi katika ukuaji wa uchumi wa Afrika. Amesisitiza kuwa wanahitaji kushiriki na kuhamasisha nchi, washirika, jamii na mtu mmoja mmoja, kufikia hatua ya kutokomeza magonjwa haya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako