Viongozi wa Eritrea, Ethiopia na Somalia wameahidi kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kijamii na kidiplomasia uliopatikana hivi karibuni katika nchi hizo tatu za pembe ya Afrika.
Hatua hiyo imekuja wakati rais wa Eritrea Isaias Afwerki, Waziri wa mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo jana kukutana huko Asmara nchini Eritrea kwa lengo la kuimarisha Zaidi uhusiano wa kidiplomasia. Viongozi hao watatu walipitisha mpango wa pamoja wa Utekelezaji wa 2020 na kuangalia Zaidi malengo makuu mawili ya kuunganisha Amani, utulivu na usalama pamoja na kuhimiza maendeleo ya uchumi na jamii. Ikwa kama sehemu ya mpango wa utekelezaji vingozi hao wa nchi tatu pia wamekubali kuimarisha juhudi za pamoja kwa ajili ya ushirikiano wenye ufanisi wa kikanda.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |