• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Askari wa kulinda amani wa UM watumwa kusaidia Mali

  (GMT+08:00) 2020-01-28 19:46:33

  Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali wamepelekwa karibu na mpaka na Mauritania ili kusaidia majeshi kufuatia shambulizi la hivi karibuni ambalo limesababisha vifo vya askari 20 wa vikosi vya serikali.

  Bw. Stephane Dujarric ambaye ni msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amesema kuwa mkuu wa ujumbe huo Bw. Mahamat Saleh Annadif amesisitiza tena kujitolea kwa mashirika ya dunia kusaidia amani na utulivu nchini Mali.

  Hadi sasa hakuna kikundi kilichotangaza kuhusika na shambulizi hilo, lakini ripoti zinasema kuna dalili kuwa limefanywa na kundi la jihadi lenye uhusiano na al-Qaida, ambao wamekuwa wakifanya mashambulizi kama hayo katika maeneo ya magharibi nchini Mali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako