• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NBC yazindua mpango maalumu wenye lengo la kuwajengea uwezo wajasiariamali

    (GMT+08:00) 2020-01-29 19:51:26
    Benki ya Biashara ya NBC Tanzania imezindua mpango maalumu wenye lengo la kuwajengea uwezo wajasiriamali nchini Tanzania.

    Kauli hiyo ilitolewa katika mkutano wa kwanza wa wanawake wa Kiislam kuhusu ujasiriamali na Tanzania ya viwanda na mkuu wa kitengo cha wateja maalumu rejareja wa NBC, Ashura Waziri.

    Ashura alisema kupitia mtandao wa Klabu ya Biashara ya NBC, wajasiriamali wanawake hususan wanaoanzisha biashara na wenye shauku ya kuanzisha viwanda, wanayo fursa ya kujiunga na klabu hiyo ili kunufaika za mafunzo yanayotolewa bila malipo kuhusu mbinu za ujasiriamali kwa vitendo.

    Semina hiyo iliandaliwa kwa uratibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) na kudhaminiwa na NBC.

    Akihutubia zaidi ya wanawake 3,000, Ashura alisema wamewajengea uwezo wajasiriamali wengi kwa kutoa mafunzo hayo yanayofanywa kwa ushirikiano na taasisi za umma na binafsi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako