Akizungumza na radio China kimataifa, Mwenyekiti wa Chama cha Wenye Viwanda, Biashara na Kilimo (TCCIA) wilayani Moshi Bw Louis Mbuya amesema benki hiyo ikisogeza huduma zake vijijini wakulima wengi wataweza kulima kwa tija na kuwa na uhakika wa mavuno ambayo ni malighafi tosha kwa viwanda vya ndani na nje ya nchi.
Alisema miaka ya nyuma wakulima wa kahawa walikuwa wakinufaika na Chama Kikuu cha Ushirika (KNCU) kwa kupewa pembejeo, lakini siku hizi hawatoi hivyo benki ya wakulima ndio itabaki kuwa mkombozi.
Aliongeza kuwa kama TADB itajisogeza kwa wakulima, viwanda vingi vitakavyoanzishwa vitakuwa na uhakika wa kupata malighafi ndani ya nchi kutokana na wakulima wengi kulima kisasa hivyo kuwa na uhakika wa mazao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |