• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wasaka dola bilioni moja za kimarekani kwa ajili ya msaada wa kibinadamu nchini Ethiopia kwa mwaka 2020

    (GMT+08:00) 2020-01-30 17:31:08

    Umoja wa Mataifa, serikali ya Ethiopia, na wadau wao wamezindua mpango wa kukusanya dola za kimarekani bilioni moja ili kukabiliana na mahitaji ya kibinadamu nchini humo kwa mwaka huu wa 2020.

    Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema, mpango huo unalenga kuwasaidia watu milioni 7 kati ya watu milioni 8.4 wanaohitaji msaada wa kibinadamu nchini humo. Amesema inatarajiwa kuwa watu waliokimbia makazi yao kutokana na mapigano, mlipuko wa magonjwa, uhaba wa mvua katika sehemu za nchi hiyo pamoja na mafuriko katika sehemu nyingine vitaendelea kuongeza mahitaji ya kibinadamu nchini Ethiopia kwa mwaka huu.

    Hivi sasa Ethiopia inakabiliwa na uvamizi mkubwa wa nzige wa jangwani, tatizo linaloweza kusababisha kupoteza maisha na uhaba wa chakula kama halitadhibitiwa mapema.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako