• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jeshi la Somalia na Marekani lashambulia kambi ya Al-Shabaab kusini mwa nchi hiyo

  (GMT+08:00) 2020-01-30 17:31:27

  Jeshi la Somalia kwa kushirikiana na vikosi vya Marekani limeshambulia kambi ya Al-Shabaab kusini mwa nchi hiyo.

  Msemaji wa serikali ya Somalia Ismael Mukhtar Omar amesema, hakuna raia waliouawa ama kujeruhiwa katika shambulizi hilo la anga katika mji wa Jilib unaokaliwa na kundi la Al-Shabaab.

  Amesema wiki hii, jeshi la Somalia na wenzi wake wa kimataifa limefanya operesheni kadhaa za kijeshi kwa mafanikio ndani na pembezoni mwa mji wa Jilib.

  Kndi la Al-Shabaab bado linadhibiti baadhi ya maeneo ya kusini na katikati ya Somalia, na linaendelea kufanya mashambulizi makubwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu pamoja na maeneo mengine.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako