• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzanite waenda Uganda kibabe

  (GMT+08:00) 2020-01-30 17:43:29

  Kikosi cha timu ya soka ya taifa Wanawake wa chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite, kimeondoka Tanzania leo kuelekea Uganda ili kuwakabili wenyeji wao katika mchezo wa kusaka tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia Vijana zitakazofanyika baadaye mwaka huu nchini Panama. Uganda wanatarajia kuwakaribisha Tanzanite katika mchezo wa marudiano utakaochezwa jumamosi kwenye Uwanja wa KCCA, Lugogo, jijini Kampala. Tanzania itashuka dimbani ikiwa na ushindi wa mabao 2 – 1 walioupata katika mechi ya kwanza iliyochezwa Januari 19 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako