• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa WHO apongeza juhudi za China katika kudhibiti virusi vipya vya korona

    (GMT+08:00) 2020-01-30 18:12:07

    Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Bw. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema, China inastahili kupongezwa na kuheshimiwa na jamii ya kimataifa kwa kuchukua hatua kali sana katika kudhibiti mlipuko wa virusi vipya vya korona na kuzuia visienee nje ya China.

    Bw. Tedros amesema hayo alipokutana na wanahabari mjini Geneva baada ya ziara yake nchini China.

    Bw. Tedros amewaambia wanahabari kuwa, hivi sasa watu zaidi ya elfu sita wameambukizwa virusi vipya vya korona vinavyosababisha ugonjwa wa nimonia, na nchi na sehemu 16 duniani zimethibitisha kuwa na maambukizi hayo. Bw. Teros amesema, hii leo ataitisha mkutano wa kamati wa dharura ili kuamua kama maambukizi ya virusi vipya vya korona yatakuwa tukio la dharura la afya ya umma duniani.

    (Sauti 1)

    "Tutaitisha mkutano wa kamati wa dharura kujadili kama maambukizi ya virusi vipya vya korona yatatangazwa kuwa tukio la dharura la afya ya umma duniani, na pia kutafuta ushauri wao kuhusu jinsi ya kulinda usalama wa watu wa dunia nzima. Hivi sasa, China inatekeleza hatua za umakini mkubwa na hatuwezi kutaka zaidi."

    Bw. Tedros amesema, alimaliza ziara yake China sasa hivi, na alitiwa moyo sana katika mazungumzo yake na rais Xi Jinping wa China.

    (Sauti 2)

    "Rais Xi Jinping anafahamu vema maambukizi ya virusi, na hata amejituma kuongoza kazi za kukabiliana na virusi, jambo ambalo limenitia moyo sana. Naona hii imeonesha uongozi mzuri wa kipekee. Kama alivyosema, hatua zinazochukuliwa na China sio tu zinanufaisha China, bali pia dunia nzima."

    Bw. Tedros amesema anapongeza juhudi kamili zinazofanywa na China katika kudhibiti virusi.

    (Sauti 3)

    "Ninaipongeza China sana, kwani hatua zinazochukuliwa na China kweli zimesaidia kupunguza kuenea kwa virusi vipya vya korona kwenda nchi nyingine. "

    Wakati huohuo, Bw. Tedros amesisitiza tena umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika kudhibiti maambukizi ya virusi.

    (sauti 4)

    "Natoa wito kwa nchi zote wanachama kufuatilia katika mambo ya siasa na teknolojia, hii inaweza kutusaidia kuzuia kuenea kwa virusi hivyo na kuvidhibiti haraka iwezekanavyo. Msingi wa kutatua changamoto hii inayoikabili dunia nzima ni mshikamano na ushirikiano."

    Habari kutoka Wizara ya Biashara ya China zinasema hadi kufikia Jumatano, China ilikuwa imetenga dola za kimarekani bilioni 3.94 kuunga mkono vita dhidi ya virusi vipya vya korona kote nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako