• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FAO yaonya tishio la kutokuwa na uhakika wa chakula pembe ya Afrika kutokana na mlipuko wa nzige

    (GMT+08:00) 2020-01-30 19:46:00

    Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO,imeonya kwamba kuna tishio kubwa la kutokuwa na uhakika wa chakula na maisha kwenye pembe ya Afrika kutokana na mlipuko wa nzige na mazalia mapya ya wadudu hao hatari.

    Ripoti hiyo iliyotolewa wiki hii inasema kuwa hali inatarajiwa kuwa mbaya zaidi kutokana na mazalia mapya ya wadudu hao ambayo yanaongeza idadi ya nzige nchini Ethiopia,Kenya na Somalia.

    FAO inasema Sudan Kusini na Uganda ziko katika hatari na pia kuna hofu ya makundi mapya ya nzige Eritrea, Sudan,Yemen,na Saudi Arabia.

    Kwa mujibu wa FAO huu ni mlipuko mbaya zaidi wa nzige wa jangwani kuwahi kutokea katika ukanda wa pembe ya Afrika kwa miongo kadhaa.

    Maelfu ya ekari za mimea na malisho yameharibiwa nchini Kenya,Ethiopia na Somalia na kusababisha wafnyabishara na wakulima wengi kupitia kipindi kigumu cha uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako