• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Tanzania yatoa hakikisho la kulinda viwanda vya ndani

    (GMT+08:00) 2020-01-30 19:46:41

    Waziri wa Viwanda na Biashara, Tanzania,Innocent Bashungwa amesema wizara hiyo imejipanga kulinda viwanda vya ndani kwa kuongeza kodi kwa bidhaa kutoka nje, lakini pia kusaidia wafanyabiashara kuibua viwanda na kuchangamkia fursa za biashara ndani na nje ya nchi.

    Bashungwa alisema mkakati huo wa serikali ni kuhakikisha wafanyabiashara wanaibua viwanda na kufanya biashara katika soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na la Pamoja Afrika.

    Alisema katika kuhakikisha Mpango wa Kuboresha Mfumo wa Udhibiti wa Biashara Nchini (Blueprint) iliyoandaliwa na serikali inafanya kazi vizuri, hivi karibuni muswada utaletwa bungeni ili kuweka mazingira rafiki ya wafanyabiashara nchini na kutumia fursa za nje pia.

    Alikuwa akijibu swali la msingi la Mbunge Magige aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kulinda biashara za wazalishaji wa ndani ili kuwajengea uwezo kuelekea uchumi wa viwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako