• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utafiti wa Benki ya Dunia waonyesha kuwa kiini cha ufukara nchini Kenya ni sera duni na ajira isiyo rasmi

    (GMT+08:00) 2020-01-30 19:47:12
    Utafiti mpya nchini umebaini kuwa kiini cha ufukara nchini Kenya ni sera duni zinazowabagua wamiliki wa biashara ndogondogo na za kati pamoja na ajira isiyo rasmi.

    Kulingana na ripoti mpya ya Benki ya Dunia kuhusu Michakato ya Thamani kuhusu uzalishaji, ukosefu wa ajira rasmi ndicho chanzo cha ufukara na kudhoofika kiuchumi miongoni mwa waajiriwa katika sekta ya kilimo nchini Kenya.

    Aidha, uchunguzi huo uliohusisha tafiti 49 kuhusu uzalishaji bidhaa ulidhihirisha kwamba "ukosefu wa urasmi ndio ukawaida badala ya kuwa suala la kipekee: Idadi kubwa ya wafanyakazi hawana kandarasi rasmi hata katika kampuni rasmi."

    Utafiti huo ulijumuisha data iliyokusanywa kutoka kwa wakulima 1,200 kutoka Kenya, Ghana na Zambia wanaokuza nafaka na ulidhihirisha kwamba Kenya inaongoza barani Afrika kwa idadi ya waajiriwa wasio na kandarasi ikifuatiwa na Zambia.

    Ripoti hiyo aidha ilionyesha kuwa asilimia 97 ya wafanyakazi katika sekta ya kilimo nchini Kenya hawana kandarasi ikifuatiwa na Zambia kwa asilimia 82. Hata kwa waajiriwa walio na kandarasi, asilimia 86 wana kandarasi zisizo rasmi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako