• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania yachukua hatua kupambana na uvamizi wa nzige

  (GMT+08:00) 2020-01-31 09:20:31

  Waziri Mkuu wa Tanzania Bw. Kassim Majaliwa amesema Tanzania imechukua hatua za kuzuia nzige wa jangawani kutoka nchi jirani.

  Akiongea bungeni mjini Dodoma, Waziri Mkuu Majaliwa amesema mamlaka tayari zinafanya mawasiliano na Kenya kuangalia namna ya kupambana na uvamizi wa nzige, wanaokula chakula na mimea. Waziri Mkuu Majaliwa amesema hayo kufuatia kundi la nzige kuvamia Kenya na Uganda na kuharibu hekta kadhaa za chakula.

  Tarehe 22 Januari waziri wa kilimo wa Tanzania Bw. Japhet Hasunga alisema serikali ya Tanzania imechukua tahadhari kubwa baada ya nzige hao kuvamia Kenya. Alisema kwa sasa kipaumbele ni kupambana na nzige hao kwenye mikoa ya mpakani, na kutaka hata mikoa isiyo mpakani kuwa makini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako