• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Bruno Fernandes asaini dili nono la miaka mitano na Manchester United

  (GMT+08:00) 2020-01-31 09:28:07

  Bruno Fernandes amesema atajitolea kwa kila hali ili kuhakikisha ushindi na kombe katika Manchester United baada ya kujiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitano na nusu akitokea Sporting Lisbon. Kiungo huyo mwenye miaka 25, amejiunga kwa dili la euro milioni 55 lakini nyongeza inaweza kulipandisha na kufikia jumla ya euro milioni 80. Meneja Ole Gunnar Solskjaer amesema kiungo huyo atasaidia pakubwa. Uhamisho wa Fernandes umejumuisha dili kubwa Zaidi katika ligi hadi sasa kwenye dirisha la uhamisho la Januari ambalo linaishia leo Ijumaa. Anawafuata Cristiano Ronaldo, Nani na Marcos Rojo kwa kujinga na Manchester United kutoka Sporting. Mkataba wake ambao utaendelea hadi mwaka 2025, pia una kipengele cha kuongeza mwaka mmoja Zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako