• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya leo

    (GMT+08:00) 2020-01-31 17:13:46

    Uingereza inatarajiwa kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya leo saa sita usiku kwa saa za Brussels, Ubelgiji kwa mujibu wa makubaliano, na itakuwa ni nchi ya kwanza kuondoka katika Umoja wa Ulaya katika historia.

    Mchakato wa kujitoa kwenye Umoja huo uliodumu kwa miaka mitatu na nusu unakamilika leo, ambapo pia utakuwa ni mwanzo wa uhusiano wa aina mpya kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya katika siku za mbele.

    Baada ya kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya, Uingereza itakuwa na kipindi cha mpito cha miezi 11 hadi tarehe 31 Desemba. Katika kipindi hicho, pande hizo mbili zitafanya mazungumzo kuhusu uhusiano baina yao, ambapo ajenda kubwa itakuwa ni kufikia makubaliano ya biashara huria.

    Hata hivyo muda wa miezi 11 ni mfupi kwa kukamilisha mazungumzo hayo, na matokeo yake yatajulikana baadaye..

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako