• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Aina 17 za unga marufuku Kenya

    (GMT+08:00) 2020-01-31 19:42:05
    Serikali imepiga marufuku aina 17 za unga wa mahindi ikisema ni hatari kwa afya ya binadamu.

    Shirika la Ubora wa Bidhaa (KEBS) lilieleza kuwa uchunguzi wake ulionyesha unga huo una viwango vya juu vya sumu hatari ya kuvu (aflatoxin), na likaagiza kampuni husika ziuondoe kwenye maduka yote.

    KEBS ilitaka aina hizo za unga zikome kuuzwa madukani kote na ikawatumia wafanyibiashara wa maduka makubwa barua pepe ikiwataka watume aina ya unga walio nao na idadi yake ili kuwezesha shirika hilo kuukusanya na kuuondoa madukani.

    KEBS ilitangaza kuwa mfanyibiashara yeyote ambaye ataendelea kuuza aina hizo za unga zilizopigwa marufuku atakamatwa.

    Mnamo Novemba 2019 KEBS ilipiga marufuku uuzaji wa unga wa Kifaru kutoka kampuni ya Alpha Grain Limited kutokana na viwango vya juu vya kuvu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako